Kuhusu Mimi Kiswahili - Wideangles Photography

Direkt zum Seiteninhalt

Kuhusu Mimi Kiswahili

About ME

Karibu sana kwenye websaiti yangu

 

Mimi niko mpiga picha kwa moyo mzima.

 

Kamera - nionavyo mimi - ni chombo tu mikononi mwa mpigapicha. Ukiangalia vyombo vya camera na camera yenyewe, utajifunza kusudi la mpigapicha mwenyewe kwa vyombo vyake, bali si kwa matokeo ya mwisho, yaani picha.

 

Nafikiri mpigapicha stadi anaweza kuumba picha nzuri na camera yoyote. Na mpigapicha mbaya hawezi kabisa kupata picha nzuri hata akiwa na camera bora.

 

Kama jicho nzuri kwa picha kwa jumla litakutana na vyombo vizuri - basi, utaona tofauti.

 

Nionavyo mimi mtu ambaye hana uso nzuri kwa picha yake hayupo. Halafu nastaajabia uzuri uliyo nyuma ya watu hawa. Kazi yangu ni kuonesha uzuri huu wazi.

 

Bahatimbaya kwangu, niliye mpigapicha na mwanasanaa ni: 99 % za kazi zangu siwezi kuonesha kwa hadharani, kwa sababu zipo chini ya amri ya siri ya uganga. Ni madaktari tu na wagonjwa wenyewe ambao wataona picha hizo. Lakini hii hainizuwii kuendelea, bali inanichochea kuonesha kwa kila mmoja ambaye ana shida au upunguvu fulani uzuri ule katika mtu huyo.

 

Hapa inakutana imani, ufundi na mazowezi. Mara nyingi napiga picha za watu, ambao wana upunguvu moja au hata zaidi.

 

Hapo naona wajibu wangu kwa watu wote.


Zurück zum Seiteninhalt